Swahili (Kiswahili) Nondiscrimination Statement

Chuo Kikuu cha Iowa kimekataza ubaguzi katika ajira, programu, na shughuli za elimu kwa misingi ya mbari, imani, rangi, dini, asili ya kitaifa, umri, jinsia, ujauzito, ulemavu, taarifa ya kijenetiki, hali kama mkongwe wa Marekani, huduma katika jeshi la Marekani, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, upendeleo wa kiushirika, au ubainishaji wowote mwingine unaombagua mtu binafsi. Chuo kikuu pia kinathibitisha ahadi yake kutoa fursa sawa na ufikiaji sawa kwenye huduma na vifaa vya chuo kikuu. Kwa maelezo zaidi kuhusu sera ya kutobagua, wasiliana na Mkurugenzi, Ofisi ya Fursa Sawa na Utofauti, Chuo Kikuu cha Iowa, 202 Jessup Hall, Mji wa Iowa, IA 52242-1316, 1-319-335-0705 (Sauti), 1-319-335-0697 (TDD), diversity@uiowa.edu.