Tumia huduma yetu ya video ili homa yako au dalili za COVID-19 zikaguliwe

Ongea na watoaji wa huduma ya afya kwa kutumia simu au kompyuta yako ukiwa nyumbani.

Ikiwa una dalili za mafua au wasiwasi wa kiafya inaohusiana na Novel Coronavirus ya wa 2019 (COVID-19), unaweza kupanga ziara ya video na mmoja wa watoa huduma ya afya.

Dalili zinaweza kujumuisha:

 • Homa katika masaa 24 iliyopita
 • Kikohozi kipya au kinachozidi na kuongezeka
 • Maumivu kwenye koo inaendelea kuwa mbaya
 • Upungufu wa kupumua inaendelea kuwa mbaya

Kutumia huduma ya video kupitia smartphone yako au kompyuta inapunguza hatari ya kupitisha ugonjwa kutoka kwa mtu hadi mtu. Utapata matibabu ya uangalifu bila kuondoka nyumbani kwako. Uangalifu kutumia huduma za video ni haraka, rahisi, na salama.

Watoa huduma wa afya watakuuliza maswali kuhusu dalili zako na watakuonyesha hatua zozote za kufuata zinazohitajika.


Jinsi ya kupanga miadi

Panga miadi kwa kupiga simu:

1-319-384-9010

Au panga kuhudumiwa kupitia njia ya video na MyChart:

Enda kwa MyChart

Pata MyChart

Kwa Vifaa vya Apple Kwa Vifaa vya Android

Kwa msaada wa dharura, tafadhali piga simu 911 mara moja.

Anzisha kuhudumiwa kupitia njia ya video

 1. Unaweza kuanza kwa kupiga simu 1-319-384-9010
 2. Au unaweza kuingia kwenye MyChart
  • Kwenye MyChart, gusa “Panga miadi”.
  • Chagua “huduma ya video: Mafua na Novel Coronavirus ya 2019 (COVID-19)”.
  • Jibu maswali fupi juu ya dalili yako.
  • Chagua wakati inafaa kwa miadi yako.
  • Kamilisha eCheck In.

Utapokea maagizo jinsi ya kutumia video na huduma salama tunayotumia ya video. Fuata maagizo hayo kisha uwe tayari kukutana na muuguzi wako kwa wakati uliochagua.


Malipo

Huduma za afya kupitia video

Ikiwa hauna bima

Huduma ya Afya ya UI itapunguza gharama ya mfukoni wakati wa mkurupuko wa magonjwa ya janga. Hutalipizwa gharama ya huduma kupitia njia ya video kwa matibabu ya COVID-19. Huduma yoyote zaidi ya huduma kupitia video itakuwa chini ya michakato ya malipo yako ya kawaida. Jifunze njia zingine ambazo zinaweza kusaidia kifedha kwa huduma yako ya matibabu.

Ikiwa una bima

Kiasi fulani inalipwa kabla ya kupokea huduma hiyo

Mpango yako ya bima itaamua kiasi fulani unayolipa kwa huduma kabla ya kupokea dhima hiyo. Bima nyingi zimetoa sehemu za wagonjwa kwa huduma hizi. Sio lazima kulipa wakati wa kuhudumiwa. Malipo ya kawaida yatatarajiwa kulipwa kabla ya kurudi kwenye huduma wa ufuatiliaji.

Mipango mingi ya bima itashughulikia na sehemu ya matibabu. Utalipa baadaye kama kuna malipo nyingine yoyote. Ili kuelewa gharama yako, tafadhali wasiliana na muuguzi wako wa afya. 

Ikiwa tutagundua kuwa huduma za video ya televisheni haifai kwa hali yako, hakutakuwa na malipo, na muuguzi atakusaidia katika kutambua hatua ambazo zitakusaidia.

COVID-19 Test

Gharama ya mtihani ya COVID-19 katika chumba cha majaribio ni $190. Kampuni za bima katika jimbo lote la Iowa, pamoja na Medicare, Medicaid, Wellmark, Aetna, na Huduma ya United Healthcare zimekubaliana kugawa gharama za kushiriki ikiwa upimaji wa COVID-19 inahitajika.

Kwa wagonjwa wasio na bima, Huduma ya Afya ya UI itapunguza gharama ya malipo kutoka mfukoni ya wagonjwa wakati huu wa janga.

Gharama ya mtihani la COVID-19 inaweza jumuisha katika malipo, gharama zingine za utunzaji wa matibabu zinazohusiana na ugonjwa wako zitategemea bima yako. Gharama hizi za matibabu zinaweza kujumuisha huduma zingine, kama vile kupima homa au magonjwa mengine ya kupumua.

Nani anastahiki?

Huduma za video zinapatikana kwa mtu yeyote mwenye umri wa miezi 2 na zaidi. Watoto wanahitaji kuwa na akaunti yao wenyewe ya MyChart.

Ikiwa unaishi Iowa, hospitali ya Chuo Kikuu cha Iowa wana uwezo wa kukuhudumia kiafya wakati wa ziara yako kupitia njia ya video.

Ikiwa hautaishi katika Iowa tafadhali ongea na muuguzi wako.

Masaa za huduma kupitia video

Siku ya juma Saa za kazi
Jumapili 7 a.m. hadi 5 p.m.
Jumatatu 7 a.m. hadi 7 p.m.
Jumanne 7 a.m. hadi 7 p.m.
Jumatano 7 a.m. hadi 7 p.m.
Alhamisi 7 a.m. hadi 7 p.m.
Ijumaa 7 a.m. hadi 7 p.m.
Jumamosi 7 a.m. hadi 5 p.m.


Kwa Kingereza