Upimaji wa COVID-19 au Dalili za shida ya upumuaji

Ikiwa una dalili za COVID-19 au umeathiriwa na COVID-19, panga ratiba au uchunguzwe kupitia njia ya video fanya miadi hapa Mychart

Ikiwa wewe si mtumiaji wa MyChart, piga simu nambari 1-319-384-9010 au jiandikishe leo.

Zifuatazo ni dalili:

 • Homa au kuhisi baridi katika masaa 24 iliyopita
 • Kikohozi kipya au inaendelea vibaya
 • Maumivu ya Koo mpya au inaendelea vibaya
 • Upungufu wa kupumua au inaendelea vibaya
 • Msongamano wa sinus au homa kali
 • Maumivu ya tumbo
 • Kichefuchefu, kutapika au kuharisha
 • Kupoteza ladha au harufu
 • Uchovu
 • Maumivu ya kichwa

SINAHAKIKA IKIWA NINAPASWA KUPANGA RATIBA?

Unaweza kuangalia dalili zako na kuchukua hatua zifuatazo MyChart.

Angalia dalili zako kwenye MyChart

Piga simu nambari 1-319-384-9010 ikiwa wewe hautumii MyChart.

Jinsi ya kupanga ratiba ya kibinafsi ya mtihani wa COVID-19

 • Kwenda kwenye MyChart.
 • Chagua COVID-19 ukaguzi wa kibinafsi.
 • Jibu maswali kwenye ukaguzi wa kibinafsi.
 • Panga jaribio la COVID-19 kupitia njia video kulingana na matokeo yako ya ukaguzi wa kibinafsi.

Nani anastahiki?

Vipimo vya kibinafsi vya COVID-19 kupitia MyChart inapatikana kwa watu wote kuanzia umri wa miezi 6 na zaidi na kwa wale ambao wana akaunti ya MyChart. Watoto wanahitaji kuwa na akaunti yao ya MyChart. Kwa watoto chini ya miezi 6, unapaswa kuwasiliana na mtoa huduma wako wa msingi. Ikiwa mtoto wako hana akaunti ya MyChart, ni rahisi kuanzisha.

Kutoka kwenye jaribio, haraka

Ikiwa unahitaji jaribio la COVID-19, tunachaguzi za kufuatilia ili kuhakikisha unapata huduma unayohitaji haraka iwezekanavyo.

 • Utapata matokeo yako kati ya masaa 24.
 • Utapata mapendekezo ya madawa au utunzaji unaohitaji baada ya mtihani.
 • Utakuwa na ruhusa kuingia kwenye programu yetu ya ufuatiliaji wa nyumbani, ambayo inaruhusu wagonjwa wa COVID-19 ambao wanastahili kukaa nyumbani wakati wanapokea huduma yao.

Anza sasa. Ingia kwenye akaunti yako ya MyChart na ujibu maswali kwenye kijikaguzi chako cha kibinafsi.

IIkiwa huna akaunti ya MyChart, ni rahisi kuanza.

Je! Huna programu ya MyChart? Ipate kwenye kifaa chako:

Piga simu 1-319-384-9010 panga ratiba

KUMBUKA

Kwa ajali za kutishia maisha na uitaji wa msaada wa dharura, tafadhali piga simu 911 mara moja.

Malipo

Ziara ya Video ya Telehealth

Ikiwa hauna bima

Huduma ya Afya ya UI haitakulipisha kwa malipo ya mfukoni wakati wa janga hii ya COVID-19. Hutalipizwa kwa gharama ya ziara yako ya video ya afya ya COVID-19. Huduma yoyote zaidi ya ziara ya telehealth itawekwa chini ya michakato ya kawaida ya utozaji. Jifunze zaidi kuhusu njia mbali mbali za ufadhili wa matibabu yako.

Ikiwa una bima

Kulipa pamoja

Mpango wako wa bima itaamua malipo yako ya kulipa pamoja au bima ya ushirikiano inawezekana kuwa ya kiwango gani. Bima nyingi zinaweza kuondoa sehemu za malipo kwa huduma hizi. Sio lazima ulipe wakati wa ziara yako ya kupata huduma. Malipo yako ya kawaida ya ushirikiano yatatarajiwa kulipwa wakati wa huduma kwa maagizo na ziara za kufuatilia.

Malipo

Mipango nyingi ya bima zinaweza kulipa sehemu ya ziara ya matibabu. Utalipizwa baadaye kwa tofauti hiyo, kama vile ungelipizwa kwa ziara zingine zozote. Ili kuelewa gharama yako, tafadhali wasiliana na wauguzi wako wa afya.

Ikiwa tutaamua kuwa ziara ya video ya telehealth haifai kwa hali yako, hakutakuwa na malipo, na mtoa huduma atakusaidia kutambua hatua zinazo hitajika

Jaribio la COVID-19

Malipo ya jaribio ya COVID-19 ni $ 201katika Chuo Kikuu cha Iowa ya Huduma ya Afya. Kampuni za bima kote jimbo la Iowa, pamoja na Medicare, Medicaid, Wellmark, Aetna, na United Healthcare wamekubali kuondoa kugawana gharama ikiwa upimaji wa COVID-19 ni lazima na muhimu

Kwa wagonjwa wasio na bima, Huduma ya Afya ya UI itaondoa malipo ya mfukoni wakati wa janga la COVID-19.

Wakati gharama ya mtihani wa COVID-19 inaweza kulipwa, gharama zingine za matibabu zinazohusiana na ugonjwa wako itategemea bima yako. Gharama hizi za matibabu zinaweza kujumuisha huduma zingine, kama vile kupima mafua, paneli ambayo inahusika na virusi vingi, na magonjwa mengine ya kupumua.

Maelezo ya ziada kuhusu bima ya afya na coronavirus inapatikana kutoka Idara ya Bima ya Iowa

Angalia habari ya bei ya Huduma ya Afya ya UI kwa homa (mafua) na paneli ambayo inahusika na virusi vingi.

Angalia habari zaidi juu ya COVID-19.

Kwa Kingereza